Tunakupa unachohitaji sasa na baadae

Propellerads
  • WELCOME TO Adonisstunner Blog FOR UPDATED NEWS AND ENTERTAINMENTS

    Search

    Jumanne, 27 Desemba 2016

    HISTORIA : SANDA ILIYOTUMIKA KUMZIKA YESU INATEGUA KITENDAWILI CHA MUONEKANO WAKE.

    "...kwa kuwa watu wengi wametia mikono kuandika mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu, kama walivyohadithiwa wale waliokuwa mashahidi kuyaona......... nimeona ni vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa hayo mambo tangu mwanzo, kukuandikia taratibu............. upate kujua uhakika wa mambo yale uliyofundishwa..."
    Luka 1: 1 - 4.

    Cesare Borgia na Sura ya Yesu.

    Cesare Borgia alikuwa ni mtoto wa nje wa Papa Alexander VI (1492 - 1503) ambaye alizaa na hawara yake aliyeitwa Vanozzza dei Catanei.

    Baada ya Borgia kufikia umri wa miaka 18 baba yake Papa Alexander VI alimfanya kuwa moja ya makadinali katika eneo la Italia ambalo lilikuwa chini ya utawala wa Papa.

    Baadae Borgia alikuja kukumbwa na kashfa kubwa ya kumuua kaka yake aliyeitwa Giovanni kutokana na wivu. Moja, Borgia alisikia wivu kwasababu kaka yake alipandishwa cheo kuwa Jemedari wa majeshi ya Papa lakini pili ulikuwa ni wivu wa mapenzi kwani wote wawili walikuwa wanajihusisha kimapenzi na mke wa mdogo wao aliyeitwa Giofre.
    Kashfa hii ilichangia kumfanya Borgia kuingia katika historia ya kuwa Kadinali wa kwanza kujiuzuru wadhifa huo.

    Baadae mfalme wa Ufaransa Louis XII alimfanya Borgia kuwa mtawala wa eneo la Valentinois na hii ndio ilikuja kupelekea kuitwa jina la utani la 'valentino'.

    Katika historia iliyoandikwa kwenye kitabu chaTriptych of Poisoners. Inaeleza kwamba mwaka 1503 Borgia alimuajiri Leonardo da Vinci kuwa muhandisi katika jeshi lake. Katika kipindi hiki pia Leonardo pia alikuwa anaendela na kazi zake za uchoraji.

    Kuna habari zinaeleza kwamba kuna uwezekano kuwa Leonardo na Borgia waliingia katika uhusiano wa mapenzi na hii inadhihirishwa zaidi na 'obsession' ya Leonardo juu ya Borgia.

    Katika picha zote ambazo leonardo alichora kuhusu Masihi Yesu Kristo alipofika hatua ya kuchora uso, alichora sura ya Borgia.
    Kutotokana na umaarufu wa Leonardo na ushawishi ambao Borgia alikuwa nao Vatican, ilikuja kukubaliwa kwa picha mojawapo ya picha za Yesu (yenye sura ya Borgia) ikawekwa ndani ya kasri la Papa.


    Cesare Borgia


    Mfano wa picha ya Yesu iliyochorwa na Leonardo da Vinci ikiwa na sura ya Borgia

    Kitendo hiki cha 'Picha ya Yesu' kuwepo ndani ya Kasri la Papa ndicho kilichangia kuenea kwa sura ya Borgia kukubalika kuwa ni sura ya Yesu.

    Hata ilipofika karne ya 20 na walipotokea watu wanatengeneza Filamu kuhusu maisha ya Yesu alitafutwa mtu ambaye anafanana na sura ya Yesu inayokubalika na kuaminiwa na wengi (Sura ya Borgia).

    Kwahiyo kwa maneno mengine hii 'Sura ya Yesu' tuliyonayo vichwani mwetu ni Sura ya Borgia ambayo iliigizwa na Brian Deacon.
    Ndio kusema Brian Deacon alipata nafasi ya kuigiza kwa kuwa ndiye muigizaji ambaye sura yake inarandana na Cesare Borgia.

    Je, Sanda ya maziko ya Yesu (Shroud of Turin) inatengua kitendawili cha 'Sura halisi ya Yesu'?



    Kuna kitambaa kirefu kimehifadhiwa katika Kanisa maarufu la 'Cathedral of Saint John The Baptist' nchini Italia katika mji wa Turin. Kitambaa hiki kinaaminiwa na wengi kuwa ni sanda aliyozikiwa Masihi Yesu Kristo mara baada ya mwili wake kuondolewa msalabani.

    Historia inaonyesha kwamba kitambaa hiki kilianza kuongelewa katika nyanja za kidini/imani miaka ya 1390.

    Madaktari wa kujitegemea wa Forensic waliokipima kitambaa hiki wametoa conclusion kwamba kitambaa hicho kinaonyesha kuwa kilifunikwa kwa mtu aliyekuwa na urefu kati ya futi 5 na inch 7 mpaka futi 6 na inch 2.

    Pia aliyefunikwa kitambaa hiki madaktari wamedhihirisha kwamba mtu huyo alikuwa na majeraha makubwa viganjani, na miguuni (misumari ya kuangikwa msalabani). Pia alikuwa na majeraha kwenye paji la uso (Taji la miba), michirizi ya damu mikononi na jeraha kubwa ubavuni (Yesu alichomwa mkuki ubavuni akiwa msalabani yakatoka maji na damu).

    Pia kitambaa hiki ina sura ambayo

    haionekani kwa macho ya kawaida na haikuwahi kujulikana kama ina picha isiyoonekana kwa macho mpaka pale miaka ya karibuni walipopiga picha ya 'negative' ya kitambaa hiki ikajitokeza sura ya mwanaume mwenye nywele ndefu, ndevu na mustachi. (Tazama picha chini).



    Picha ya negative ikionyesha sura ndani ya should of turin.

    Kuna utata mkubwa kuhusu kitambaa/sanda hii.. Kwani pia wanasayansi walitumia teknolojia ya Carbon 14 kupima umri wa kitambaa hiki na kugundua kwamba kilitengenezwa (kilianza kuexist) miaka 800 tu iliyopita (1200's).

    Kwahiyo watu wanaopinga kuwa hii si sanda ya Yesu hii ni moja ya hoja zao kuu kuwa kama kweli ilikuwa ni sanda ya Yesu Carbon 14 ilipaswa kuonyesha kina miaka si chini ya 2000.

    Lakini wanaotetea kuwa hii ni sanda ya Yesu wanadai kuwa ni impossible kutengeneza kitu cha kugushi cha kiwango hiki.

    Kwa mfano sura kwenye kitambaa hiki inaonekana pekee ukitumia vyombo vya teknolojia vinavyotoa picha ya 'negative' hii inamaanisha image imejipandikiza ndani ya kitambaa (sio juu au nyuma).

    Wako wanasayansi wanaosema kuwa ili utengeneze kitu cha kugushi cha kiwango hiki unapaswa kutumia mionzi maalumu (atomic laser) teknolojia ambayo haikuwepo kipindi hicho cha miaka ya 1200's.

    Mjadala kuhusu 'sanda ya Yesu' ni mkali mno.
    Kanisa katoliki halijawahi kuikataa au kuikubali rasmi kama hii ni sanda halisi ya Yesu.

    Lakini mwaka 1958 Papa Pius XII aliikubali Sura iliyoonekana kwenye kitambaa hiki kuwa ndiyo Sura halisi ya Yesu. Na Papa John Paul II amewahi kutamka kuwa kitambaa hiki 'Shroud of Turin' kinaakisi injili/kioo cha injili ("a mirror of the gospel)
    Papa Francis alipotembelea eneo la hifadhi ya Should of Turin

    Muhimu: Tujadili kwa staha tukiheshimu imani za wengine.



    =================
    Vatican

    Inasemekana Yule mama Veronika anayesimuliwa katika biblia aliyemfuta Yesu USO sura ilibaki katika kitambaa Na kuwa kile kitambaa bado kipo. Kuna ukweli kuhusu hilo?

    Kuhusu kitambaa cha Veronika (sio sanda ya Yesu shroud of Turin)

    Hapana, kuna ukweli nusu tu kuhusu hilo.

    Ukweli:kwa mujibu wa historia ya kanisa katoliki kitambaa hiki kinachojulikana kama 'The veil of veronica' au Sudarium kwa kilatini.. Inasemekana Mtakatifu Veronika alimpa Yesu ajifute jasho na damu kipindi amebeba msalaba anapelekwa Golgotha kusulubiwa na baada ya Yesu kujifuta alipomrudishia huyu mama kwa namna ya kimiujiza image ya sura yake ilibakia.

    Baada ya hapo kipindi chote hiki kitambaa hiki kilihifadhiwa Vatican na mara ya mwisho kuonekana ilikuwa ni mwaka 1436.

    Uongo: si kweli kwamba kitambaa hiki bado kipo mpaka Leo..
    Mwaka 1527 Mji wa Roma uliingia kwenye machafuko makubwa na sehemu kubwa ya Vatican ikaharibiwa. Hapo ndipo hiki kitambaa kilipotea.

    Baada ya hapo watu wakaanza kutengeneza copy za kile kitambaa mitaani. Mwaka 1616 Papa Paulo V akapiga marufuku kutengeneza copy za kitambaa cha Veronika mitaani. Lakini akaruhusu kitengo maalumu kilichopo ndani ya Vatican (Saint Peter's Basilica) kutengeneza copy za kitambaa cha Veronica.

    Miongo kadhaa baadae, mwaka 1629 Papa Urban akaingia madarakani na akapiga marufuku kabisa kutengenezwa copy za kitambaa cha Veronica iwe ndani ya Vatican au nje. Na copy zote zilizokuwapo zilichomwa moto.

    Mpaka leo hii Vatican hakuna kitambaa cha Veronica Original wala copy..

    ====================

    Matola
    Ni out of topic lakini nijibu hapahapa, kwenye last supper aliyochora huyu Da Vinci wale wote ni mitume wake 12? Au ni kweli Da vinci amemuweka na mwanamke mmoja? Nikiangalia image zinanichanganya sana.
    Hebu nidadavulie kwa usahihi kipengele hiki tu cha last supper

    Mchoro wa last super una vitendawili vingi sana na nadharia nyingi sana! Nieleze zile ambazo zinanivutia na angalau zina chembe chembe au dalili kwa mbali kuwa zinaweza kuwa na ukweli..

    - kwanza kabisa tufahamu kuwa kuna vitabu kadhaa (mfano the holy blood and the holy grail & the templar revelation) vinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa Leonardo da Vinci alikuwa ni member wa kikundi cha Prior of Sion kikundi ambacho kihistoria kinasemekana ndio kinajua siri ya Holy Grail (holy grail ni kifaa kama kikombe ambacho kihistoria inasemekana kiliachwa na yesu kwa wanafunzi wake, kina siri nzito kuhusu imani, ufunuo na 'blood line' ya masihi)

    - sasa katika biblia inaelezwa kuwa siku ya last supper Yesu kwanza aliubariki mkate kisha akauvunja kuwapa wanafunzi wale, baada ya hapo akabariki divai kisha akawapa wanafunzi wanywe..
    Tukirudi kwenye mchoro, utaona kwamba vipande vya mkate vipo lakini hakuna kikombe cha divai.. Sasa nadharia hii inaeleza kwamba Leonardo alikuwa anajaribu kuuambia ulimwengu kuwa Holy Grail sio kifaa kama kikombe kama wanavyodhani. Swali: kama sio kikombe, holy grail ni nini??

    - ukiangalia katikati ya Yesu na mwanafunzi aliyekaa mkono wa kulia wa Yesu (mkono wa kushoto kwa unayeangalia picha) utaona kwamba Leonardo amewachora akaacha katikati nafasi ambayo inatengeneza umbo la 'V'. Vikombe vya divai enzi hizo za Yesu vilikuwa na shepu hii ya V. Kwahiyo kinachoelezwa ni kwamba Holy grail ni "jambo" ambalo lipo katikati ya Yesu na huyu aliyekaa pembeni mwa Yesu na kifaa kama kikombe kama ilivyoaminiwa kwa miaka mingi.. Conclusion inakuja kwamba Holy grail ni Mary Magdalena. Swali: kwanini Mary Magdalena???

    - ukichunguza maandiko kuna wanawake walikuwepo kwenye 'tafrija' ya last super lakini unapofikia hatua ya kushiriki kwenye mlo wenyewe wa last supper maandiko hayaonyeshi kwamba walishiriki.
    Sasa nadharia hii inaeleza kwamba Mary Magdalena alikuwepo kwenye last super na alishiriki na siri hii ilijulikana na wachache hasa hasa member wa kikundi cha Prior of Sion ambacho Leonardo inasemekana alikuwa mwanachama.

    Hii ndio sababu wengi wanadhani ilimfanya Leonardo amchore mwanafunzi aliyekaa mkono wa Julia kwa Yesu (mkono wa kushoto kwa unayetazama picha) amemchora katika muonekano tata akiwa na sura ya kike kabisa.
    Kwa miaka mingi imeaminika kuwa huyu ni mwanafunzi yesu aliyempenda sana (Yohana) lakini wenye kuamini nadharia hii wanakanusha wanasema leonardo amemchora Mary Magdalena.

    - nadharia hii inawekewa uzito zaidi na wanaoiamini kwa kufananisha mavazi ya Yesu na wanafunzi wake wote wengine. Utakuja kugundua kuwa Leonardo amemchira Yesu na aliyekaa mkono wake wa kulia mavazi yao yakiwa yana randana kabisa tofauti ikiwa ndogo mno!
    Suala hili la Leonardo kumchora yesu na aliyekaa mkono wake wa kushoto kufanana kwa mavazi inaelezwa kuwa Leonardo alikuwa anajaribu kuuambia ulimwengu kuwa kulikuwa na 'romance' kati ya wawili hao.

    - Pia miaka ya karibuni mwanamuziki nguli kutoka Italia anayeitwa Giovani, ameeleza kuwa ukiangala kwa makini jinsi vipande vya mikate vilivyolo mezani na jinsi Leonardo alivyochora position za mikono za yesu na wanafunzi wake unapata alama za kimuziki.
    Na kama utasoma alama hizo kutoka kulia kwenda kushoto (Leonardo alikuwa anapenda kuandika kutoka kulia kwenda kushoto badala ya kushoto kwenda kulia japokuwa alikuwa anaandika kilatini) hivyo ukisoma alama hizo kwa mtindo wa kutoka kushoto kwenda kulia unapata 'nota' ya muziki (music note) na wengi wanaamini nota hii ni code ambayo ikiwezekana kuwa 'cracked' basi tutapata siri nyingine ambayo Leonardo alikuwa anajaribu kuieleza.

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    Search

    Chapisho Lililoangaziwa

    NEW HIT:OMMY DIMPOZ FT ALIKIBA-KAJIANDAE

    Toa Maoni yako

    Jina

    Barua pepe *

    Ujumbe *

    Wanaofuata

    Propellerads