Kama kuna taifa ambalo gharama ya kulilinda ni kubwa hata gharama ya kuendesha maisha ni Hii ISRAEL ya sasa Iliopo eneo lililojulikana kama Parestina (according to Roman empire). Gharama hii sio ya kifedha tu inaenda mbali hadi kuwa gharama ya UHAI.
Hebu tumuangalie Huyu mmoja Eliyahu ben Shaul Cohen na kazi iliyotukuka aliyolifanyia taifa lake wenda tukajifunza nini maana ya Uzalendo kwa vitendo.
MAISHA YA AWALI
Cohen alizaliwa Alexandria Misri na familia ya Kizayuni, Baba yake(myahudi mzarendo) akihamia mji huo akitokea ALEPPO (WOte tunajua Mji huu ambao umekuwa maarufu kwa vita thidi ya ISIS huko syria), Pia Ikumbukwe eneo lote la Kuanzia Syria hadi Mpaka wa syria lilijuliakana kama Syria Parestina israel ikiwa imemezwa humo. Alijaribu kujiunga na Jeshi la Misri lakini kutokana na Uyahudi wake alizuiliwa, Aliacha Chuo Baada ya Kubaguliwa vijana wa MUSLIM BROTHERHOOD akiwa Chuo kikuu na kuamua kujisomea mwenyewe nyumbani. Mwaka 1947 baada ya kuanzishwa Taifa la Wayahudi/ISRAEL wayahudi wengi wakatoka misri kurudi kwao yeye akabaki amalizie masomo yake aliyokuwa anajisomea ELECTRONICS.
HUJUMA ZA AWALI HUKOHUKO MISRI
Alibaki misri kuendelea na movement za kichinichini japo alikuwa sio trained. Waliunda kikundi cha wayahudi waliohujumu Miundombinu ya Marekani na Uingereza ili kuichonganisha Misri na Ulaya na Marekani huku wakisaidiwa kwa siri na polisi wa Israel. Kikosi cha kijasusi cha wamisri kiliwagundua na baadhi walinyongwa lakini hakukutwa na hatia maana hakuwa mstari wa mbele.
KUKATALIWA KUJIUNGA NA MOSSAD
Alishiriki kuwatorosha wayahudi wengi kwenda kwao Israel wakiwemo wazazi wake, Baadae na yeye akarudi. Alijiunga na jeshi Kitengo cha Kiintelijensia Israel Military Intelligence (AMAN) baadae akaomba kazi MOSSAD. Alikataliwa na kuonekana hana vigezo. Kwa hasira akaachana na jeshi na kuwa raia wa kawaida. Kumbe kwa Muda wote ameacha kazi karibu miaka miwili amekuwa akifuatikiwa kwa karibu sana na majasusi wa AMAN. Siku ikafika ikapigwa hodi nyumbani anatakiwa Kujiandaa na MISSION kama AGENT wa MOSSAD.
COHEN NI NANI NA MAANDALIZI YA MISSION AMBAYO YANGEMGHALIMU MAISHA
Huyu namaa alikuwa mtu smart tangu utotoni. Alukuwa na uwezo karibu kila kitu. Uwezo wake mkubwa wa kutunza kumbukumbu hakukumuhitaji hata kubeba karamu na karatasi. Alianza kwa kuelekezwa jinsi ya kugundua kama mtu anamfuatilia, Alifundishwa kiarabu cha syria, akianza kuhudhuria Msikitini zaidi ya mwaka Huku akikariri mistari ya Quran ambayo Muislamu yoyote mwaminifu lazima ajue, Alifyundishwa jinsi ya kutengeneza microphone, na silaha ndogondogo. Akapewa jina la kiarabu KAMEL AMIN SABET na akaandaliwa kuwa kama mfanyabiashara mkubwa wa kisyria(Funiture). Katika silaha zake zote akili ilikuwa silaha Number Moja na ya thamani.
MISSION ILIANZIA ARGENTINA
Eli alipewa VISA kwenda kuishi argentina kama Mfanyabiashara mkubwa wa Syria kwa jina la KAMEL AMIN SABET. Argentina ilikuwa nchi yenye watu wa syria wengi wakifanya biashara huko. Alijichanganya kwenye mahoteli na migahawa na ambapo wa syria walikuwa wakikutana kama vile LA CASA ARABE nchini humo. ni huko alipokutana na mwanasiasa AMIN AL HAFIZ akiwa ktk harakati zake za kujipnaga kisiasa na kuwa marafiki wakubwa.
MISSION HALISI SYRIA NA JINSI ALIVYOKOA MAELFU YA NDUGU ZAKE HASA WALIOKUWA CHINI YA MILIMA YA GORANI.
Alifika akaishi kwenye hotel kubwa pembeni ya makao makuu ya Jeshi la Syria. Akawa anaangalia miendendo yote na kuripoti huko kwao. Akajijengea Umaarufu na watu mashuhuri hasa jeshini. Kuna kipindi alitembezwa hadi Milima ya Golan na kujua kila kitu vifalu, jinsi mambo yao yote yalivyo. Ikumbukwe kwa kipindi cha miaka 20 SYRIA walikuwa wakirusha mabomu Israel hasa maeneo ya wakulima Karibu na Golani na watu waliishi kwa wasiwasi. Huko ndiko alipodukua mpango kabambe wa kujenga bwawa ili maji yote yanayotiririka kuelekea Israel(asilimia kubwa ni jangwa) yasifike. Bwawa hilo lilishambuliwa mapema bila kujua israel wamejuaje na mpago huo ukafa. ALiendelea kujikusanyia taarifa lukuki zilizowanufaisha israel bila kujulikana.
KIFO NA MWISHO WAKE
Alipata nafasi ya kurudi Israel kisiri na kukutana na familia yake bila kujua kumbe ndio mara ya mwisho. AMIN AL HAFIZ alitoga argentina akaja kugombea na Kuwa raisi wa Syria. Kwa jinsi alivykuwa karibu na Jasusi huyu bila kujua Alifikilia kumpa UWAZIRI WA ULIZI. Kabla haya yote hayajafanikiwa siku moja kitengo cha kijasusi cha SYRIA wakisaidia na WARUSI walinasa SIGNAL za sauti zilizotia shaka. Kwa gari maalumu walianza kutrack hadi wakagundua zilikuwa zinatokea kwenye chumba ambacho Jasusi huyu aliishi. Siku hiyo alikuwa anaripoti vitu vingi wakamsikiliza kwa muda zaidi ya masaa manne na kuvamia wamachukua. Aliteswa Na kulazimishwa kutuma taarifa za uongo Israel, kwa mbinu zake aliwajulisha wenzake katikati ya mazungumzo hayuko katika mikono salama. Baadae akahukumiwa kwa kosa la Uhaini. Eli alinyongwa usiku huo katikati ya Jiji la Damscus. Asubuhi mamia ya watu walipita wakimkuta akiwa ananing'inia huku amewekewa bango lenye list ya makosa yake. Huo ndio ulikuwa mwisho wake.
MATUNDA YA KAZI YAKE KWA TAIFA
Pamoja na mambo mengi, siri nyingi alizozipata ikiwemo udhaifu wa jeshi la syria ambao Israel hawakujua. Miaka miwili baada ya kifo chake taarifa zake zilisaidia Ushindi mkubwa wa Israel wa vita vya SIKU SITA. Taifa la israel likajichukulia Milima yote ya Golani maana COHEN alikuwa ameisema yote na maficho ya vifaru, mahandaki na silaha nzito. Hadi leo japo vitendo vya israel haiungwi mkono na watu wengi wapenda haki, Nchi hiyo ipo salama kwa mchango wa watu wachache waliojitolea uhai wao.
Source.MSEZA MKULU JF.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni