Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu mbunge Wa Mbeya mjini amenusurika kifo baada ya gari lake kufeli bleki na kumgonga mtoto wa miaka 15 aitwae Rachel ambapo mtoto alifariki dunia wakati akikimbizwa hospitali.
Mh. Sugu alikuwa akielekea uwanja wa ndege Songwe ndipo alipo fika maeeneo ya Iyunga akapata ajali hiyo mbaya japo yeye na dereva wake hawajapata madhara yeyote mpaka gari hilo lilipo weza kusimama eneo la Tazara Mbeya.
Aidha gari la polisi lilolokuwa likienda kutoa msaada eneo la ajali hiyo ya Mh. Sugu nalo limepata ajali na kupinduka huku askari wake wanne Kati ya sita waliokuwepo wakijeruhiwa.
Search
Jumamosi, 17 Desemba 2016
Habari
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni