Mazoezi kwa wanaume huongeza mbegu za uzazi
Watafiti wamesema ni muhimu kufanya mazoezi kwa kiwango cha wastani.
Mazoezi ya nusu saa mara tatu kwa wiki kwa wanaume yana uwezo wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mujibu wa wanasayansi
Wanaume ambao wameendelea na zoezi la kukimbia kila wakati , mbegu zao huwa na afya njema, kulingana na watafiti wa jarida la maswala ya uzazi.
Watafiti wamesema ni muhimu kufanya mazoezi hayo kwa kiwango cha wastani , kwa sababu mazoezi ya kupita kiasi hudhuru kiwango cha uzalishaji wa mbegu hizo za kiume.
Utafiti umebaini kwamba wale wanaoshiriki katika michezo kama vile ya uendeshaji baiskeli wanauwezo wa kupunguza kiwango cha mbegu zao za uzazi.
Mbinu za kuongeza mbegu za kiume:
Weka korodani katika madhari mazuri, kwa kuepuka kuvalia suari za ndani za kukaza.
Usioge na maji moto sana.
Epuka magonjwa ya zinaa.
Wacha uvutaji wa sigara.
Punguza kiwango cha pombe.Usinone sana.
Fanya mazoezi, lakini kwa kiwango cha wastani.
Wanaume wote 261 waliosajiliwa katika majaribio hao hawakuwa na matatizo yoyote ya kiafya au shida ya uzazi. Walikuwa na kiwango sawa cha bengu za uzazi na zilizokuwa na afya, na walioishi maisha bila kufanya mazoezi.
Wanaume hao walishirikishwa kwenye mradi mmoja kati ya miradi minne ikiwemo:
Kutofanya mazoeziMazoezi makali mara tatu kwa wiki (dakika moja ya mbio ya kasi na mapumizo mafupi katika kila dakika kumi)Mazoezi wa wastani mara tatu kwa wiki ( dakika 30 katika mashine ya kufanyia mazoezi) Mazoezi makali , mara tatu kwa wiki.
Mafunzo ya mazoezi yalionekana kuongeza kiwango cha mbegu za uzazi zilizo na afya huku waliofanya mazoezi yaliowastani walipata matokeo bora zaidi.
Wanaume wote katika makundi matatu walipunguza uzani wao na walipata matokeo bora ikilinganishwa na wanaume ambao hawakufanya mazoezi kwa wiki 24 katika kipindi cha majaribio.
Watafiti wamesema manufaa waliopata wanaume hao ni kutokana na kupunguza uzani katika makundi matatu ,wote walipunguza kiwango cha mafuta kutoka kwa miili yao.
Watafiti tayari wamebaini kwamba unene kupita kiasi unaweza kusababisha shida za uzazi. Robo tatu ya wanaume hao walikuwa na uzani kupita kiasi.
Huduma ya kwanza ya kuimarisha mbegu za uzazi ni gani?
Kile kitu ambacho hakijajulikana ni iwapo mazoezi huchangia kuimarisha mbegu za uzazi. Hili ni jambo ambalo watafiti wanahitajika kuchunguza zaidi kwenye mahabara kuchunguza iwapo mazoezi huchangia katika ongezeko la mbegu za uzazi.
Mtafiti mkuu Behzad Hajizadeh Maleki amesema, '' kulingana na matokeo hayo yamebaini kwamba kufanya mazoezi inaweza kuwa mbinu rahisi, na bora ya kuimarisha mbegu hizo za uzazi kwa wanaume ambao wanachangamoto za uzazi.''
''Hi bayana kukiri kwamba wanaume wengine hawapati watoto si kwa sababu ya ukosefu wa viwango vya mbegu zao za kiume.
Shida za uzazi kwa wanaume zinaweza kuwa kubwa na iwapo wanaume wataweza kubadili njia zao za kuishi zinaweza kukabiliana na shida hizo kwa urahisi.'' kwa mujibu wa Prof. Allan Pacey wa chuo kikuu cha Sheffield.
Uingereza umewasihi watu wazima kufanya mazoezi kwa dakika 150 , kama vile kuendesha baiskeli , au kutembea kwa haraka, ama dakika 75 ya mazoezi yanayotumia nguvu kama vile kukimbia kila wiki.
Source :Bbcswahil
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni