Watu sita (06) wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda aina ya Canter lenye namba za usajili T 634 ADF lililokuwa likitokea mnadani Mlalo kwenda Soni.
Gari hilo lilipata ajali baada kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Mgaro Kata ya Mgaro Tarafa ya Mlalo wilayani Lushoto.
Waliofariki katika ajali hiyo kwa mujibu wa kamanda ni Jamali Hemedi, Khadija Saidi, Zuena Juma, Husna Athumani, Nusura Seif na Hassan Rashid.
Aidha, waliojeruhiwa wametajwa kuwa ni Seif Bakari, Sauda Shemtui, Mwanahamis Ayoub, Abeid Ayoub, Khalifa Juma, Mariam Kassim na Mwanamvua Yusuph.
Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Benedict Wakulyamba ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kupita kwenye mlima mkali wenye utelezi ulionyeshewa mvua.
Search
Jumapili, 26 Februari 2017
Habari
Habari Habari Habari
AJALI MBAYA LUSHOTO, SITA WAFARIKI ,SABA MAJERUHI,,,,
DAGAA SAFI NA WASIO NA MCHANGA KUTOKA BUKOBA Oct 15, 2017
HABARI: MKUU WA UPELELEZI AUWAWA KWA RISASIFeb 22, 2017
Labels:
Habari
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni