Tunakupa unachohitaji sasa na baadae

Propellerads
  • WELCOME TO Adonisstunner Blog FOR UPDATED NEWS AND ENTERTAINMENTS

    Search

    Jumapili, 31 Julai 2016

    UMEWAHI SIKIA YALIYOTOKEA KATIKA GEREZA LA TACUMBU NCHINI PARAGUAY

    Polisi nchini Paraguay wamegundua seli ya kifahari katika gereza la wafungwa sugu nchini humo Tacumbu.
    Seli hiyo ilikuwa ya mfungwa mmoja ambaye ni kiongozi wa genge la ulanguzi wa mihadarati.
    Katika seli hiyo ya kipekee yenye vyumba vitatu polisi waligundua mlikuwa na sebule ,maktaba, jikoni, na chumba cha kutizama televisheni.
    Mlanguzi wa mihadarati raia wa Brazil Jarvis Chimenes Pavao ndiye aliyekuwa akiishi humo na mfungwa yeyote aliyetaka kuishi naye humo alitozwa kodi ya dola elfu tano pesa taslim.
    Lakini kwanini waishi humo ?
    Mlikuwa na viti vya kifahari, yaani mwenyeji angeweza hata kutazama vipindi ya runinga, video , angeweza kuoga maji ya moto .
    Kuta yake ilikuwa imewekwa matofali ya kisasa na ya kuvutia.
    Uchunguzi umeanza kubaini ni maafisa wagani katika gereza hilo waliomruhusu mlanguzi huyo wa mihadarati kuishi maisha hayo ya kifahari humo gerezani.
    Sadfa ni kuwa mle ndani mlikuwa na video moja iliyokuwa na simulizi ya maisha ya mlanguzi hodari wa mihadarati kutoka Colombia Pablo Escobar.
    Escobar ambaye aliuawa mwaka wa 1993 alikubaliana na viongozi wa idara ya magereza nchini Colombia kuwa atakubali kutumikia kifungo chake gerezani ilimradi tu aruhusiwe kuijenga seli atakamoishi.
    Wafungwa wenzake wamehuzunishwa na ugunduzi huo wa polisi ambao wanadai umewapokonya bwana mkarimu sana humo gerezani.
    Mmoja wa wafungwe wenza bwana Antonio Gonzalez amenukuliwa akisema kuwa alikuwa maarufu sana ,na aliwapenda wote aliokutana na kujumuika naye.
    ''Alikuwa bwana mcheshi sana ''
    Mfungwa huyo tajiri wa kupindukia amehamishwa hadi katika gereza lililoko karibu na mji mkuu wa Asuncion.
    Polisi waligundua seli hiyo ya kipekee katika gereza hilo la Tacumbu baada ya kudokezewa kuwa kulikuwa na mtu aliyeagiza aletewe bomu mle ndani.
    Yamkini raia huyo wa Brazil Chimenes Pavao ambaye alikuwa anatarajiwa kukamilisha kifungo chake cha miaka minane gerezani hapo mwakani hakutaka arejeshwe Brazil, kwa hivyo alikuwa amepanga njama aletewe bomu ambalo angelitumia kulipua ukuta wa gereza hilo na kutoroka.

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    Search

    Chapisho Lililoangaziwa

    NEW HIT:OMMY DIMPOZ FT ALIKIBA-KAJIANDAE

    Toa Maoni yako

    Jina

    Barua pepe *

    Ujumbe *

    Wanaofuata

    Propellerads