Viongozi wengi wa ngazi za juu huwa wanaangalia ni jinsi gani wanaweza kujilimbikizia mali za nchi na kujijenga kwanza wao kimaisha bila kujali wananchi waliyomuweka madarakani wako katika hali gani ya maisha. Viongozi wa aina hiyo mara nyingi hupenda kujipa kipaumbele sana wao na familia zao zaidi huku wakifurahia kuishi kwa matabaka kwa vile tu wao ni viongozi.
Jose Alberto ‘Pepe’ Mujica Cordano anaheshimika sana nchini Uruguay. Na inasemekana ni Rais maskini zaidi duniani na Rais huyu aliyetumikia nchi yake kuanzia mwaka 2010 mpaka 2015 kama Rais 40 wa nchi ya Uruguay.
Kinachomfanya Mujica awe tofauti zaidi na wa kipekee kuliko Marais wengine duniani ni ukarimu wake. Uamuzi wake wa njia ya kuishi aliyoichagua ulimfanya aonekane kwa watu kwamba ni Rais maskini zaidi duniani. Aliamua kuishi kwenye shamba la kawaida kupita maelezo
lililokuwalinamilikiwa na mkewe, licha ya kuwa na uwezo wa kuingia na kutoka katika nyumba iliyotengwa kwa aajili ya Marais wa nchi hiyo, na nyumba anayoishi ni kawaida tu, na iko katika kijiji kilichopo nje kidogo ya mji wa Montevideo.
Maisha ya Mujika ni ya kustaajabisha na kuvutia kwa wakati uleule. Mshahara naolipwa kama Rais wa nchi hiyo ni kiasi cha $12,000 kwa mwezi na cha kushangaza zaidi takribani 90% ya mshahara huo unaenda kwa watu maskini wasiojiweza na anabakiwa na kiasi cha fedha cha wastani wa fedha anazopata mfanyakazi wa kawaida wa Uruguay. Na licha ya hayo yote, hajawahi kujihisi kwamba yeye nimaskini na anafurahia maisha yake ya shambani huko.

Meet the poorest president in the world and
Gari (1987 VW Beetle) yake ndo kitu chake cha thamani zaidi ambayo kwa mwaka 2010 ilikuwa na thamani ya $1,800.
Shamba aliloamua kuishi lililoko nje kidogo ya mji wa Montevideo

Alichaguliwa kuwa Rais mwaka 2009, na Mujica alitumikia kifungo cha pekee jela kwenye miaka ya 1960 na 1970 ikiwa ni adhabu aliyopewa kwa kuwa mmoja wa kundi la guerrilla Tupamaro, waliokuwa wakiibia matajiri na kuwapa maskini (Robin-Hood style) kipindi cha Mapinduzi ya Cuba.
Alipigwa risasi mwilini mara 5 na kutumikia kifungo kwa miaka 14, muda mwingi akiwa amefungiwa peke yake bila kuonana na mtu yeyote ikiwa na mazingira magumu sana mpaka alipoachiwa mwaka 1985 wakati Uruguay iliporudisha Democrasia nchini humo. Mujica anasema miaka hiyo aliyotumikia jela ilimfanya aone maisha kama anavyoyaona sasa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni