Tunakupa unachohitaji sasa na baadae

Propellerads
  • WELCOME TO Adonisstunner Blog FOR UPDATED NEWS AND ENTERTAINMENTS

    Search

    Ijumaa, 19 Agosti 2016

    MAHAKAMA YAMWAMURU REGINALD MENGI AFIKE KUJIELEZA KWANINI ASIFUNGWE KWA KUPUUZA HUKUMU YA MAHAKAMA

    MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeamuru Mwenyekiti Mtendaji waMakampuni ya IPP, Reginald Mengi afike mahakamani kujieleza kwa nini asifungwe gerezani kwa kushindwa kutekeleza hukumu inayohusu malipo ya Sh bilioni 1.2.

    Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu kujieleza kutokana na kushindwa kutekeleza hukumuiliyomtaka kuwalipa wafanyabiashara watatu, Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo, Sh bilioni 1.2.

    Alitakiwa kuwalipa fedha hizo kutokana na mgogoro wa malipo ya uuzwaji wa hisa katika Kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd ambayo kwa sasa inaitwa Handeni Gold Inc.

    Kwa mujibu wa hati ya wito wa kufika mahakamani, Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu ili ajieleze kwa nini asifungwe gerezani kama mfungwa wa madai kama sehemu ya kukazia hukumu hiyo.

    Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na wafanyabiashara hao kuwasilisha maombi katika hatua ya kukazia hukumu iliyotolewa Januari 28, mwaka huu na Jaji Agathon Nchimbi wa mahakama hiyo.

    Katika hati ya kiapo ya wafanyabiashara hao, inadaiwa walifungua kesi dhidi ya Mengi na Kampuni ya K.M. Prospecting Limited, wakidai malipo yaliyokuwa yamebakia ya dola 428,750, 100,000 na 70,000, kwa kila mmoja.

    Chanzo...Jamiiforum

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    Search

    Chapisho Lililoangaziwa

    NEW HIT:OMMY DIMPOZ FT ALIKIBA-KAJIANDAE

    Toa Maoni yako

    Jina

    Barua pepe *

    Ujumbe *

    Wanaofuata

    Propellerads