Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Joseph Pombe Magufuli leo hii tarehe 26/09/2016 amewasili katika bandari ya Jijini Dar es salaam
Rais amesikitishwa kukuta kuna watu wana elimu ya darasa la saba ila CV zao zikionesha wana degree,, asema kila mtu atafanya kazi kulingana na elimu yake
Pia Rais amesikitishwa kukuta mashine za kukagulia mizigo scanner mbili hazifanyi kazi, hivyo kuwataka wahusika wahakikishe mashine hizo zinafanya kazi mara moja, na kuwapa miezi mitano wawe wameongeza scanner mpaka kufikia sita,,
Amewataka TPA, TRA, usalama/Polisi kuwepo wote kwenye scanner hizo ili kuepusha ripoti zinazotofautiana.
Mkataba wa TICTS ulikuwa wa miaka 10 lakini Ikaongezwa mingine 15 kinyemela ametaka TPA na TRA kupitia upya mkataba huo..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni