Tunakupa unachohitaji sasa na baadae

Propellerads
  • WELCOME TO Adonisstunner Blog FOR UPDATED NEWS AND ENTERTAINMENTS

    Search

    Jumanne, 13 Septemba 2016

    WANAMUZIKI WA HIPHOP (10) MATAJIRI ZAIDI DUNIANI..

    Wiki hii gazeti la forbes la nchini marekani limetoa orodha ya wasanii wa Hip Hop wenye mkwanja zaidi Duniani,,,, 

    Ambapo katika chati hiyo mwanamke yupo mmoja peke yake 
    Orodha ni kama ifuatavyo hapa chini 👇👇👇👇👇👇

    01.DIDDY

    Mbali na mziki Diddy ametengeneza fedha nyingi kwa miradi mbalimbali nje ya mziki kama mkataba wa kutengeneza vinywaji vya Diageo's Ciroc Vodka
    Kinara huyu anamiliki dola za kimarekani millioni 62
    02.JAY Z

    Anazidi kutengeneza hela na kampuni yake ya Rocknation entertainments pamoja na kampeni mbalimbali anazoziendesha 
    Anamiliki kiasi cha dola za kimarekani millioni 53.5
    03.DR DRE

    Mwaka jana aliachia albamu yake kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya kumi kupita pia kutoa ngoma kali ndo kuliko muongezea mapato zaidi 
    Anamiliki kiasi cha dola za kimarekani millioni 41

    04.DRAKE

    Amekuwa ni msanii wa Hip Hop mwenye mauzo mazuri ya kazi zake, pia dili za Apple, sprite na Nike zimemuongezea "chapaa" 
    Anamiliki kiasi kisichopungua dola za kimarekani millioni 38.5

    05.WIZ KHALIFA

    Anamiliki kiasi cha dola za kimarekani millioni 24 ,Show zake 70 ndo zilizomuongezea mapato zaidi. 

    06.NICK MINAJ

    Ni mwanamke pekee kwenye orodha na amezidi kuitetea nafasi yake hiyo anamiliki dola za kimarekani millioni 20.5, Tour za pinkprint ndo zilizomlipa zaidi,,,, 

    07.PITBULL

    Anamiliki kiasi cha dola za kimarekani dola millioni 20, na ndiye msanii aliyeingia mkataba na lebo za biashara nyingi katika kutangaza biashara ukiachia mbali snop dog,, ameingia mkataba na lebo kama Playboy ,Norwegein cruise Lines na nyingine nyingi

    08.PHARRELL WILLIAMS

    Huyu anamiliki kiasi cha fedha kisichopungua dola za kimarekani million 19.5 ,anapiga mkwanja mrefu baada ya kuwa miongini mwa wamiliki wa kampuni ya G-star Row

    09.KENDRICK LAMAR
    Ameshika na nafasi ya Tisa kwa kumililiki mkwanja usiozidi dola za kimarekani millioni 18.5 kutoka na shoo anazopiga na Lucrative festival gigs pamoja na mkataba aloingia na kampuni za Reebok pamoja na Calvin klein. 

    10.BIRDMAN. "BABY"



    Huyu ni msanii ambae kwa mwaka huu hajauza sana albamu zake ila kiwanda chake cha mziki "Cash Money Records" bado kinamuingizia mpunga wa kutosha,,,, anamiliki kiasi cha fedha kisichopungua dola za kimarekani millioni 18..

    ××××××

    Nimekuwekea pia video toka forbes iliyowapanga kwenye list,,,,,, 

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    Search

    Chapisho Lililoangaziwa

    NEW HIT:OMMY DIMPOZ FT ALIKIBA-KAJIANDAE

    Toa Maoni yako

    Jina

    Barua pepe *

    Ujumbe *

    Wanaofuata

    Propellerads