Nchi inayokumbwana vita na ile inayoongozwa kwa ukandamizaji wa jeshi kwa miongo kadhaa ndio mataifa yanayotajwa kuwana atu wakarimu zaidi duniani, utafiti umeashiria.
Raia wa Iraq ndio wana roho za imani zaidi huku wale wa Myanmar wakitajwa kuwa wakarimu zaidi kwa mujibu wa orodha ya mataifa yenye ukarimu ya CAF mwaka huu 2016.
Katika mwezi uliopita, raia 8 kati ya 0 wa Iraq wamewasaidia watu wasiowajua, huku Libya pia ikilingana sawa kwa hilo.
Katika wakati huo huo, 91% ya raia wa Myanmar wametoa pesa za misaada.
Ikilinganishwa na 63% ya raia wa Marekani - taifa la pili kwa ukarimu kwa jumla - wamechanga pesa, huku 73% wakidai kumsaidia mtu wasiyemjua.
Orodha hiyo ya kila mwaka imeiweka Myanmar, juu ya orodha kwa mwaka wa tatu mtawalia, ikiwa na nusu ya idadi ya watu nchini wanaotoa usaidizi kwa watuna 63% wakiwasaidia watu wasio wajua.
Ripoti hiyo inasema ukarimu huo unadhihirisha utamaduni wa "Sangha Dana", ambako waumini wa Kibudhaa huwasidia watu wasiojiweza kimaisha.
Orodha hiyo kwa jumla inayozingatia usaidizi wa fedha, na usaidizi wa kujitolewa, unaiorodhesha Uingereza juu miongoni mwa mataifa ya Ulaya kwa ukarimu, Umoja wa falme za kiarabu katika mashariki ya kati , Kenya barani Afrika na Guatemala huko Amerika ya kusini.
China imeorodheshwa chini kwa ukarimu.
Mataifa 10 yalio na ukarimu zaidi dunianiNambariNchiUkarimu kwa jumla1Myanmar70%2Marekani61%3Australia60%4New Zealand59%5Sri Lanka57%6Canada56%7Indonesia56%8Uingereza54%9Ireland54%10Umoja wa Falme za Kiarabu53%
"Licha ya kuwashuku awali watu wasiowajua, raia Libya wana utamaduni wa kuvutia katika ukarimu," anaeleza mwandishi wa BBC wa Afrika kaskazini Rana Jawad.
"Katika uzoefu wangu hili lilidhihirika zaidi baada ya kutimuliwa madarakani Gaddafi; Kumekuwa na mtazamao tofuati wa ukarimu wa raia Libya kabla ya mapinduzi wa 2011, sio kuwa hawakuwa wakarimu wakati huo, lakini walihofia kuwasaidia watu wasiowajua.
"Baada ya mapinduzi , raia walikuwana ukarimu zaidi. mzozo nchini humo ndio huedna umechangia nafasi ilioorodheshwa Libya kwasababu kwa kukosekana maafisa wa usalama, kumewalazima raia kutegemeana kwa usaidizi."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni