Hivi hili la walimu ni kubwa kuliko matukio
mengine nchini? Ukitaka kujua kunya anye kuku akinya bata kaharisha basi chukua tukio hili linalovuma sasa nchini kuhusu walimu mafunzoni waliomuadhibu mwanafunzi huko mbeya.
Kila mtu anasema lake kila raia anasema lake
kisa kuna jina mwalimu, nauona ukandamizaji na udhalilishaji, hili si kubwa kuliko mengine
yaliyopo na yaliowai kuwapo nchini..
Leo media ndio mjadala, nimeamka asubuhi
mada ni hii redioni, kwenye tv, magazeti na hukowhasapp na kwingineko ndio usiseme.
Hivi waandishi wa habari mna weledi kweli?
Hivi Kipigo cha mtoto ambae hata hajajeruiwa ni kikubwa kuliko watafiti waliouwa Dodoma?
Ni kikubwa kuliko Kifo cha Mwangosi mikononi
mwa Polisi?
Mbona mijadala haikufika hapa, wala
hatukumuona mawaziri watatu mpaka wanne
wakisimama ndani ya masaa machache baada
ya uvumi/tukio kutoa matamko na hukumu kwa
watuhumiwa?
Hivi hili limewauma sana serikali kuliko
mengine? Kwanini haikuwa busara liende kwa taratibu za kisheria mpaka mahakamani walimu hawa waliokuwa mafunzoni wapewe haki yao na chombo cha kutoa haki?
Siwezi sema walichotenda walimu hawa ni sawa lakini je hatua za hukumu pia zipo sawa?
Tunasikia hadi vyuo wameshafukuzwa, je hii ni
hukumu ya haki?
Mbona scorpion aliemtoa mtu macho sijasikia
hata waziri mmoja akisema auwawe? Au
alichofanya scorpion, wale wanakijiji wa dodoma kuwauwa watafiti ni zuri kuliko hili?
Watanzania tuache mihemuko, na ndio maana
nchi hii ina wanafiki wengi, wasioweza kuhoji
wala kuchanganua wapo kumfurahisha fulani
wapate vyeo, fulani nae yupo kutoa tuzo kwa
kila mnafiki.
Lazima ifike wakati tuishi ndani ya haki na
kweli.
Wengine wanasema yani katoto kadogo vile
walimu watano? Mbona hamuulizi yani vi walimu viwili tu vilivyopo mafunzoni mawaziri watatu na
waandishi wa habari wote wamesimama? Na
wakiungwa mkono na Watanzania kibao
Hali halisi zilizopo Mashuleni:
Wengi hamjui hali halisi zilizopo mashuleni,
walimu wenzangu wanajua sana tena vema hali
halisi mashuleni, na hali mbaya ya utovu wa
nidhamu mashuleni, ambayo imeletwa na serikali ya kuchanganya siasa na taaluma.
Wanafunzi wanajua wana haki kubwa sana
mashuleni kuliko walimu, kama hamjui mlijue
hilo, siku hizi watoto hawafukuzwi mashuleni
maana siasa za wanasiasa na sera za serikali
zinasema watoto wabembelezwe wamalize
shule.
Ndio maana michujo na mitihani kama ya kidato cha pili haipo, lengo ni amalize shule hayo mengine si ya muhimu kabisa kabisa
Viboko na adhabu za kawaida ni haramu shuleni,
serikali haina msimamo thabiti, waraka wa
adhabu uliopo hauna mwanya wa kutoa adhabu
za maonyo kwa wanafunzi, leo linatokea hili
nchi inasimama, kweli?
Nitoe mifano halisi mwaka jana kuna walimu
walikuja mafunzoni shule nnayofundisha,
wanafunzi wawili wakamshika matiti mwalimu
wa kike alipokuwa darasani, mwalimu
alifadhaika sana. Tukatoa adhabu kwa hawa
watoto ya suspension (kurudishwa nyumbani) na viboko vinne kila mmoja.
Usiku ule ule wakamvizia mwalimu mwingine wa kiume alie mafunzoni alieonesha kuguswa na tukio wakampiga mawe na akapasuliwa juu ya jicho.
Hivi katika mazingira haya unafanya nini? Nani
ana wajibu wa kumlinda mwalimu dhidi ya
watoto na jamii iliooza? Sisemi wanastahili
kipigo kiasi kile ila nataka kila anaesoma hapa
achukue nafasi ya Mwalimu. Na ajiulize kama
yeye ni mwalimu angejiteteaje na wapi?
Sisi tunakutana na mengi msioyajua, watoto
hawa ni wala bange, anakuja shuleni asubuhi
kala bangi, kanywa viroba na anakuona
mnalingana, huwezi kumwambia kitu, unaweza
kuwa unafundisha yupo bize na kipenzi chake
wanafanya yanayowapendeza, ukichukua hatua
hata ya kupeleka ofisi ya nidhamu basi wewe ni
mnoko bifu zinahamia mtaani/kijijini mnakoishi.
Na kadri mtoto mmoja anapoharibikiwa na shule inashindwa kumfukuza (kwasababu ya Siasa)
wanaiga waliopo nyuma yake. Tunaishi katika
vijiji na miji ambapo walimu ni adui namba moja wa jamii kama tu mwalimu huyo ataonekana ana deal na nidhamu vema. Hata kesi utazushiwa za uongo.
Nitoe mfano mwingine, wiki tatu zilizopita
nilikuwa na adhibu watoto waliochelewa namba
nikiwa zamu, nilipofika kidato cha nne niliadhibu wote isipokuwa mtoto mmoja nilipomfikia akasema sitaki, mie huwa sichapwi, nikatoka nje lakini nimefedheheshwa sana.
Chukua nafasi yangu alafu uamue, ukimwangalia ni mtoto wa kumzaa kabisa ama mdogo wako wa mwisho, vipi ukiwa na hasira katika mazingira kama hayo?
Ndio maana nasema watanzania tunakurupuka
na kuongea bila kutazama pande zote hili
hukumu ya haki ipite.
Walimu wanastahili haki yao lakini pia ni wakati
walimu walindwe dhidi ya watoto wakorofi ama
serikali iweke mazingira ya adhabu na watoto
walioshindikana.
Wapo walimu waliokwisha zira kabisa wao
wame declare kufundisha tu hata mtoto apande
juu ya bati hawatamgusa kwakuwa mtoto
analindwa kuliko mwalimu, hivi mtoto
aliekushika matiti utaendelea kufundisha akiwa
hapo shuleni?
Yapo mengi siwezi kuandika yote ila walimu
wanajua vema sana mambo haya, wanajua
kadhia zinazowakabiri usiku na mchana, kupigwa mawe mitaani, kurushiwa mayai viza, kuzushiwakesi vijijini kwakuwa tu anachukua hatua za nidhamu haya watu hawayaoni,
Mnaona tu kilichomkuta mtoto ambae hata hajalazwa hospitali.
Kesi za mimba hasifiki mbali kwakuwa walimu
uamua kuachana nazo, maana jamii
inakubaliana wanayamaliza na mwalimu
unaefatilia utakiona cha moto.
Ninyi watanzania huko mitaani, bar, na makazini kwenu hamshikani mashati kwa hasira za ubinadamu? Mbona kwa walimu owe kioja?
Hivi la walimu ni dhambi kuliko la Scorpion
alietoa macho watu na hakupewa hukumu ya
hapohapo kafikishwa kwenye vyombo vya
sheria?
Mwalimu ni mwanadamu kama walivyo wengine wote.
Ukweli utasimama daima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni