Taarifa kutoka maeneo ya kusini mashariki mwa Nigeria, zasema kuwa watu 60 wameuwawa pale paa la jengo moja la kanisa kuporomoka katika mji wa Uyo.
Taarifa zasema kuwa, kuna watu wengi ambao wamekwama ndani ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Ajali hiyo imetokea wakati mamia ya waumini walipokuwa wakihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa muasisi wa kanisa la Reigners Bible, Akan Weeks kama askofu
Ujenzi wa majengo ya Kanisa hilo ulikuwa bado ukiendelea, huku serikali ikitangaza kuwa itaanzisha uchunguzi kubaini ikiwa utaratibu wa ujenzi mwema ulikiukwa au la.Wakati wa mkasa huo, gavana wa jimbo laAkwa Ibom, Udom Emmanuel, alihudhuria ibada hiyo, kwa pamoja na wanasiasa wa eneo hilo, ambao waliepuka ajali hiyo.
Source BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni