MAMBO KUMI NA TANO (15) YALIYOTOKEA KWENYE MKUTANO MKUU WA TAIFA WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) JANA, 21 AGOSTI 2016.
Na. Mtatiro J
1. Akidi ilitimia pande zote, Bara na Zanzibar na mkutano ulimchagua Ndugu. Julius Mtatiro kwa kura takribani 500 kuwa Mwenyekiti wa Kikao, alifuatiwa na Ndugu. Ridhiwani wa Morogoro aliyekuwa na kura takribani 170 na hivyo nduguMtatiro alipitishwa rasmi kuongoza mkutano.
2. Mkutano Mkuu kwa kauli moja ulipitishaajenda mbili: Moja ni Taarifa ya Barua yaKujiuzulu kwa Prof. Lipumba na mbili niUchaguzi wa Kujaza nafasi wazi za Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa na Wajumbe wanne wa Baraza Kuu.
3. Mkutano Mkuu ulianza ajenda ya kwanza chini ya Uenyekiti wa ndugu Mtatiro ambapoKatibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alipewa ruhusa ya kueleza taarifa yakujiuzulu kwa Prof. Lipumba na alieleza jambohilo kwa kina, hatua kwa hatua.
4. Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF wapatao 10 kutoka Tanzania Bara walitoahoja zao kwa kutaka Kikao kimuite Prof.Lipumba ili aje ajieleze kuhusu kujiuzulu kwakejambo ambalo lilipingwa na wajumbe wengine.Mwenyekiti wa kikao aliwataka wajumbewanaotaka Lipumba aletwe waweze kuelezakifungu cha katiba au kanuni kinachotakaKiongozi aliyejiuzulu yeye mwenyewe aitwekujieleza, wajumbe hao walishindwa kutoamamlaka ya kikatiba au kikanuni. Wajumbe waliokataa Prof. Lipumba kuja mkutanoniwalinukuu ibara ya 117(2) ambayo inatakataarifa ya kujiuzulu kwake ndiyo ipelekwekwenye mkutano mkuu na siyo yeyemwenyewe. Mwenyekiti wa kikao aliujulisha mkutano kuwa Prof. Lipumba si mjumbe wa kikao kwa hiyo hawezi kuitwa kwa sababuyoyote ile na kwamba mkutano ujadili baruazake na ufanye maamuzi ya kumrudisha aukutomrudisha.
5. Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu waCUF kutoka Tanzania Bara walikataa Mkutano Mkuu usifanye maamuzi yoyote. Wajumbe wengine wa Bara walitaka maamuzi yafanyike, kwa hiyo Tanzania Bara iligawanyika nusu kwa nusu kwenye jambo hilo. Hofu ya wajumbe wa Bara waliokataa maamuzi yasifanywe ilikuwa ni kuwa yakifanyika yataathiri mipango yao.
6. Majira ya saa 8 mchana wakati mkutanoukiendelea na baadhi ya wajumbe wa barawakiomba mkutano mkuu umuite Prof. Lipumba, ndipo Profesa alipojitokeza akiwa na kundi la MABAUNSA wapatao 30wakisindikizwa na Ofisa wa POLISI aliyekuwa na RADIO CALL (Angalia picha ya ukurasa wambele gazeti la Mtanzania). Kundi hilo liliwazidi nguvu walinzi wapatao 10 waliokuwa kwenye lango kuu na hivyo Prof. Lipumba akaingiamkutanoni kwa nguvu na kuketi upande mmoja na "genge" lake. Baadhi ya wajumbe wa bara wapatao 150 hivi kati ya 320 waliohudhuriawalisimama na kushangilia ujio wa Lipumbakwa dakika kadhaa. Mwenyekiti wa Mkutanoaliwatuliza
7. Mwenyekiti wa Mkutano aliwajulisha wajumbe kwamba kwa hatua iliyopo lazimawafanye uamuzi aidha wa kumrejesheauenyekiti Lipumba au kumuondoa kabisa, kwa kupiga kura. Wajumbe walewale takribani 150wa Bara waliendelea kupinga kitendo chochote cha kupiga kura, wakitaka mkutano mkuuumuidhinishe Lipumba kurudi kwenye uenyekiti "kienyeji" na bila kutumia kura.
8. Mwenyekiti wa Mkutano alitoa OPTION ya pili kwamba Mkutano Mkuu uache ajenda ya kwanza uhamie ajenda ya pili na kufanyauchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa chama na ule wa wajumbe wanne wa baraza na kwamba Mjadala juu ya Lipumba uahirishwe na piauchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti uahirishwe. Wajumbe wa bara walewale takribani 150 katiya 320 walikataa OPTION hii ya pili wakasimama na kupiga makelele kuwaLipumba arudishwe bila uamuzi wa kikatiba wa Ibara ya 112.
9. Mwenyekiti wa Mkutano Ndg. Julius Mtatiroaliuahirisha mkutano kwa zaidi ya saa moja ili wajumbe wakapate chakula. Katika muda huo wa mapumziko viongozi wa kitaifa wa CUFwaliwasiliana na viongozi wa jeshi la Polisikuanzia kanda, mkoa, wilaya ili kujua ni kwa nini polisi waliokuwepo walimruhusu nakumsindikiza Lipumba ukumbini na kutaka kujua ni kwa nini wanashindwa kumuondoa kwa sababu si mjumbe. Polisi walieleza kuwawanao ulinzi wa kutosha hapo hotelini nakwamba mkutano ukirejea wataimarisha ulinzi na kuzuia makundi yoyote yasiyo wajumbekuvamia mkutano kama lilivyofanya kundi la Lipumba na watu wake. Polisi walikataa katakata kumuondoa Lipumba na genge lakeukumbini.
10. Mkutano uliporejea, Mwenyekiti wa kikao aliwaongoza wajumbe kufanya maamuzi ikiwa LIPUMBA aondoke au abaki kwa mujibu wakatiba ya CUF ibara ya 117 (2). Wajumbe takribani 150 wa bara walisimama na kupinga.Wajumbe takribani 130 wa bara na wajumbe takribani 340 wa Zanzibar walipiga kura nakuamua kuwa Lipumba AONDOKE RASMI.Jumla ya wajumbe waliomuondoa Lipumba nikwa kura zilizphesabiwa rasmi ni 476 huku waliosema ASIONDOKE wakiwa 14 tu.Wajumbe takribani 150 hususani kutoka Tanzania Bara walikataa kushiriki katika upigajikura lakini wasingeliweza kuathiri akidi aumaamuzi. Baada ya uamuzi huo muhimu na ukilishwaji wa ajenda ya kwanza, mwenyekiti wa kikao alikiahirisha kwa saa nzima.
11. Kikao kiliporejea saa 1 jioni hivi, Mkutano Mkuu ulihamia kwenye ajenda ya pili yaUchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Baraza.Mwenyekiti wa kikao alimkaribisha Mwenyekiti wa Uchaguzi wa ndani ya chama Wakili msomi Awadh Said akisaidiwa na Wakili msomi JobKralio ili waongoze shughuli uchaguzi. Wakili awadh alitoa taarifa ya utangulizi akawatambulisha wajumbe wa kamati yake nawakajipanga mbele ya wajumbe.
12. Wakati Wakili Awadhi (Mwenyekiti waUchaguzi) akiendelea na zoezi lake, wajumbewale 150 wa Tanzania bara walisimamawakijaribu kuzuia uchaguzi usifanyike.Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu aliwatuliza na wakamsikiliza lakini ghafla, milango mikuu ya Blue Pearl ilivamiwa na kundi la vijana zaidi ya 200 wakitokea nje, vijana hao wavamizi ambao kwa vyovyote vile lazima walikuwawamekodiwa kwa ajili hiyo, waliwazidi nguvu walinzi wetu wa mlangoni wakaingia ukumbini.
13. Polisi kikosi kizima waliokuwepo hawakufanya chochote baada ya hali hiyo,wameshuhudia makundi ya watu wasiowajumbe wakiingia ukumbini na wamewaacha wafanye hivyo bila kuwazuia. Viongozi wa Polisi waliokuwepo "walitorokea mlango wa pili" immediatelly baada ya kundi la wahunikuvamia.
Kundi lile lote likawa limo ukumbini ukijumlisha na lile kundi la Lipumba na mabodigadi wakewa kukodi. Kundi jipya la wavamizi mia mbilililianza kuleta vurumai kwa kupiga baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu (wajumbe kamwe hawakupigana wao kwa wao, hata mara moja, walivamiwa kutoka nje na wahuni na baadhi ya wajumbe kunyang'anywa viti na kupigwa aukutishiwa kupigwa).
14. Kutokana na hali hiyo majira hayo kwa mamlaka ya kikatiba aliyokuwa amepewa naMkutano Mkuu, ndugu Julius Mtatiro aliahirisha Mkutano Mkuu wa CUF hadi itakapotangazwa vinginevyo. Baada ya kuuahirisha viongoziwalilindwa na kuondoka mkutanoni kwautaratibu na wajumbe wa mkutano mkuuwakaongezewa ulinzi wa hoteli ili wawe salama.
15. Kwa maoni yangu, pamoja na kuwa Prof. Lipumba ameamua rasmi kuingia vitani nachama chake tena kwa malengo halisi ya AJENDA NA MASLAHI YAKE BINAFSI, ukweliunabakia kuwa POLISI walikuwa ni sehemu ya Mkakati wa kuuvuruga mkutano wa CUF. Kama Polisi wangelitoa ulinzi kidogo tu, mkutanoungelifanyika na uchaguzi ungelifanyika hadimwisho. Lakini USALITI wa LIPUMBA akishirikiana na VYOMBO VYA DOLA unaweza kuwa mzizi mkuu wa hali ya jana.
#Note 1: Leo nimeelezea kwa kirefu ninikilitokea mkutanoni jana. Kesho ntaeleza maoni yangu binafsi kwa ujumla.
#Note 2: Picha mbili za kwanza zinamuonesha Ofisa wa Juu wa Polisi (mwenye shati yakitenge) akimsaidia Lipumba na mabodigadiwake kuvamia Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF.
#Note 3:. Picha ya pili na ya tatu zinaoneshawajumbe Mkutano Mkuu wa CUF wakihesabiwa ili kuamua ikiwa Lipumba ANAONDOKA auANABAKI.
Mtatiro J.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni