Tunakupa unachohitaji sasa na baadae

Propellerads
  • WELCOME TO Adonisstunner Blog FOR UPDATED NEWS AND ENTERTAINMENTS

    Search

    Jumatatu, 22 Agosti 2016

    MKURUGENZI MKUU WA USALAMA WA TAIFA ASTAAFU NAFASI YAKE YAKAIMIWA NA GEORGE MADAFA

    Rais Kikwete akiwa na Rashid Othman Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.JPG

    MKURUGENZI Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Rashid Othman amestaafu rasmi wadhifa huo.

    Amestaafu rasmi wadhifa huo Agosti 19,mwaka huu akiwa ameiongoza taasisi hiyotangu Agosti 20, 2006 ikiwa ni takribanimiaka 10.

    Kiongozi huyo aliteuliwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwaMkurugenzi Mkuu ili kuziba nafasiiliyoachwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa wakati huo, Cornel Apson Mwang’onda.

    Aliapishwa Ikulu Dar es Salaam Agosti 21,2006. Kabla ya uteuzi wake, Othmanalikuwa Mkuu wa Utawala na Utumishi wa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa na kufanya kazi nzuri, iliyochangia kumwezeshakuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.

    Awali, Othman alitakiwa kustaafu mwaka2013 kwa mujibu wa sheria, lakini aliendeleakuongezewa mkataba wa mwaka mmojammoja hadi alipokubaliwa kustaafu rasmiIjumaa iliyopita. Othman atakumbukwa kwa kazi nzuri, aliyoifanya kwa Taifa tangualipoingia katika utumishi wa umma.

    Chanzo cha kuaminika kimeliambia Gazetila Mtanzania kuwa nafasi ya Rashid Othmankwa sasa inakaimiwa Mkurugenzi waMambo ya Ndani ya Idara ya Usalama waTaifa, George Madafa.


    Chanzo. Mwananchi

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    Search

    Chapisho Lililoangaziwa

    NEW HIT:OMMY DIMPOZ FT ALIKIBA-KAJIANDAE

    Toa Maoni yako

    Jina

    Barua pepe *

    Ujumbe *

    Wanaofuata

    Propellerads